“MBIO ZA MAGARI NI MUHIMU KWANGU KULIKO MECHI YA ARSENAL” HII NDIO KAULI YA KOCHA JOSE MOURINHO

Share this

Kocha wa Manchester United Jose mourinho amewashangaza wengi baada ya kuacha kwenda kutazama fainali ya FA cup kati ya Arsenal na Chelsea katika dimba la Wembely nchini wingereza.

Kocha huyo ambaye ametoka kutwaa taji la Europa League kwa mara ya kwanza akiwa na United,ameonyesha kuwa na misimamo yake binafsi baada ya kukacha fainali hiyo ya FA na kutimkia jijini Monaco katika fainali za Magari maarufu kama Formula One.

Inasemekana Mourinho alipata mualiko wa kuhudhuria fainali hizo za formula one kutoka kwa timu ya REDBULL ili kupata nafasi ya kuwatazama waendesha magari wa timu hiyo Max Verstappen na Daniel Ricciardo.

The Manchester United boss had his picture taken with Red Bull’s Max Verstappen

Although Jose Mourinho didnt look so pleased to see Daniel Ricciardo

Ikumbukwe kwamba kocha Jose Mourinho baada ya kufanikiwa kubeba kombe la Europa alitoa tamko kwamaba “sitajihusisha na mpira ndani ya mwezi mmoja na najua kwamba leo kuna fainali ya FA,lakini pia Ujerumani kuna fainali na hata Hispania,sitaki sitaki kabisa na sna hata hamu ya kupata matokeo”Mourinho pia aliongeza kwa kusema”huu ndio muda muafaka wa kuacha kabisa kufikiria mpira na kufanya mambo mengine,kuwa karibu na familia na marafiki ili nisahau mpira kwa sasa nataka iwe hivyo”

Jose Mourinho admitted he couldnt care about football over the next month

 

Dondosha comments


Share this