Morata: Nipo tiyari kuishi London kwa miaka 10

Share this

Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata amekanusha uvumi kwamba hapendi kuishi jiji la London na yupo tiyari kusaini mkataba wa miaka kumi kama itawezekana.

Awali Morata aliliambia gazeti moja la Italia kwamba hana maisha marefu katika jiji la London.

Alipoulizwa kuhusiana na kauli hiyo wakati akijiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa Jumanne dhidi ya Roma, alisema alimaanisha hatokaa London baada ya kustaafu soka.

”Nina furaha sana hapa, na ninafurahia kila kitu cha London mimi na mke wangu,”alisema.

Morata mwenye miaka 25 amefunga magoli saba katika michezo 13 tokea aliposajiliwa kwa Pauni Milioni 60 kutoka klabu ya Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitano.

Dondosha comments


Share this