MOROCCO NDIO KIKWAZO CHA IVORY COAST KUTOFUZU KWENDA RUSSIA

Ivory Coast's Chelsea team player Didier Drogba (C) celebrates his goal with other teammates during the first half of the knockout round football game between Ivory Coast and Libya at the African Nations Cup (CAN), 24 January 2006 in Cairo. AFP PHOTO ISSOUF SANOGO
Share this

Mchezo wa mwisho wa kufuzu kucheza kombe la Dunia mwakani kati ya Ivory Coast na Morocco unaotarajiwa kuchezwa mwezi ujao mjini Abidjan utakuwa zaidi ya fainali kutokana na uhitaji mkubwa wa ushindi kwa timu zote mbili

Kocha Mkuu wa Ivory Coast Marc Wilsmot  anauona mchezo huwa kuwa mgumu zaidi kutokana na hali ya timu yake ambayo inahitaji ushindi ili iweze kufuzu ilihali Morocco wakihitaji Sare tu kwenda Urusi 2018.

Ivory ambao walikuwa wakiongoza kundi C kabla ya mchezo wao dhidi ya Mali ulioisha kwa suluhu wameshuka mpaka nafasi ya pili mbele ya Morocco ambao waliwafunga Gabon goli 3.

“Tunashukuru tuliweza kupata walau pointi dhidi ya Mali, licha ya kuwa na majeruhi wengi lakini tulijitahidi kucheza kwa ubora na kumiliki mpira kwa sana dhidi ya Mali timu ambayo ni ngumu zaidi kuchezanayo hasa ikiwa nyumbani” Marc alinukuliwa

“Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa muunganiko wa viungo wale kucheza pamoja kutokana na majeruhi tuliyokuwa nayo ila nadhani tunayo fainali ya kucheza Abidjan mwezi ujao tunahitaji ushindi “aliongeza

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho Ivory Coast kushinda kwenye ardhi ya nyumbani kwenye mchezo dhidi ya Morcco ilikuwa ni June 5 mwaka 1995 ilposhinda goli 2-1

Dondosha comments


Share this