RASMI LIVERPOOL YATUMA RUFAA YA KADI NYEKUNDU YA SADIO MANE,KAZI KWA FA

Share this

Rasmi klabu ya Liverpool imetuma rufaa kwa chama cha soka cha England FA kutokana na adhabu ya kufungiwa mechi tatu iliyomkuta mshambuliaji wake Sadio Mane,Mchezaji huyo raia wa Senegal alimkanyaga kipa Ederson wa Manchster wakati Liverpool ilipokumbana na kipigo cha mabao 5-0 siku ya jumamosi na kupewa kadi nyekundu .
Image result for sadio mane and ederson

Hata hivyo tayari Mane alimuomba msamaha kipa huyo lakini FA imeamua kumfungia mechi tatu ingawa Liverpool inaona si sawa kwa kuwa tayari alipewa adhabu ya kadi nyekundu uwanjani,Liverpool imetuma rufaa hiyo kwasababu Mane ni mchezaji tegemeo katika kikosi chao kwa sasa baada ya kukosekana kwa Philippe Coutinho ambaye amepumzishwa na kocha Jurgen Klopp

Image result for sadio mane and ederson

Dondosha comments


Share this