Rasmi: Wayne Rooney amerejea Everton

Share this

Aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney muda mchache ulipita amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na club yake ya zamani ya Everton, club ambayo ilimlea tangu akiwa na umri wa miaka 9.

Wayne Rooney akisaini mkataba na Everton

Rooney ameondoka Manchester United kama mchezaji huru baada ya kuitumikia club hiyo kwa muda wa miaka 13 ambapo amecheza jumla ya michezo 559 na kufanikiwa kuifungia mabao 253.

Unaambiwa Rooney amekubali kupunguza asilimia 50% ya mshahara wake ukilinganisha na Pound 300,000 aliyokuwa akilipwa kwa wiki akiwa United hadi  PPound 150,000 anayoenda kulipwa katika club yake mpya ya Everton.

Unaweza kuona ni jinsi gani Rooney ana mapenzi na kiu ya kurudi tena katika club yake hiyo ya zamani.


 

Dondosha comments


Share this