SIMBA NA AZAM KUPIGWA SAA MOJA USIKU,TFF YATANGAZA VIINGILIO LEO

Share this

Kuelekea mchezo wa Azam FC dhidi ya Simba, Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao utapigwa Jumamosi ya wiki hii.

Image result for simba vs azam

Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex maarufu kwa jina la Chamazi ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana kwenye uwanja huo katika miaka ya hivi karibuni baada ya TFF kutangaza kuwa rasmi Azam FC inaweza kuutumia mchezo huo katika mechi zake za nyumbani dhidi ya Simba na Yanga kwa kuwa awali zilikuwa haziruhusiwi kucheza uwanjani hapo.

Related image
Viingilio katika mchezohuo vitakuwa Sh 10,000 kwa jukwaa la V. I. P na mzunguko sehemu ambayo ina uwezo wa kukaliwa na watu elfu sita kiingilio chake ni Sh 7,000,Mcchezo huo unatarajiwa kupigwa majira ya saa 1:00 usiku na itakuwa kwa mara ya kwanza timu hizo kucheza usiku katika ligi kuu Tanzania bara.

Dondosha comments


Share this