WALIOSALIMIKA KATIKA SHAMBULIO LA KIGAIDI LA MANCHESTER NI PAMOJA NA FAMILIA YA KOCHA PEP GURDIOLA

Share this

 

Image result for pep guardiola with his family

Kufuatia tukio la shambulizi la kigaidi taarifa zimetolewa leo kuwa mke na watoto wa Kocha wa Manchester City, Pep Guadiola imeelezwa walikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwapo kwenye tamasha  kwenye Ukumbi wa Ariana Grand ambapo watu 22 waliuawa huku zaidi ya watu 50 wakijeruhiwa.

Image result for pep guardiola with his family

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kupitia TV3, familia ya kocha huyo ilikuwepo wakati shambulio hilo likitokea tukio ambalo limestua dunia na kuchukuliwa kama tukio la kigaidi,Vile vile, inaelezwa kuwa baadhi ya wachezaji wa Manchester City ambao hawakutajwa majina yao walikuwepo na familia zao, lakini hawakuathiriwa na shambulizi hilo.

“Tumeshtushwa na shambulizi hilo  na tunashindwa kuamini kilichotoke. Salamu zetu za pole kwa ndugu jamaa na marafiki waliopata matatizo,” uliosomeka ujumbe huo kupitia mtandao rasmi wa twitter wa wafuasi wa Guardiola “Pep Team Tweeter”

Hata hivyo mkutano wa klabu ya Manchester United na vyombo vya habari kuhusu mechi yao ya kesho umeahirishwa huku uongozi ukisisitiza kwamba mechi hiyo ipo palepale.

Dondosha comments


Share this