ANTONY JOSHUA AJITAMBA KUWA YEYE NI BORA KULIKO BONDIA YOYOTE KWENYE UZITO WA JUU

Share this

Bondia mwenye asili ya Nigeria na raia wa Uingereza Anthony Oluwafemi Olaseni Joshua anaamini kuwa yeye ni muhimu katika tasnia hiyo na anatarajia kuwa bora zaidi kwa mabondia wa uzito wa juu.

Image result for anthony joshua

 

Anthony Joshua mwenye umri wa miaka 27 ameanza kujiandaa kwaajili ya pambano lake lijalo la kutetea ubingwa wa WBA na IBF ambapo huwenda akapambana na mpinzani wake Kubrat Pulev,Joshua amesisitiza kuwa hakutarajia kama angepata mafanikio makubwa kama aliyofikia hivi sasa katika mchezo huo kwa kuweza kutwaa mkanda wa ubingwa wa IBF kutoka kwa bondia Charles Martin mwaka jana huku akifanikiwa kuweka historia ya kumpiga kwa knocking out Wladimir Klitschko mwezi Aprili.

Image result for anthony joshua

“Wakati huo sikuwahi kufikiria kuwa naweza kuwa bingwa siku moja wakati wote nilikuwa nikifanya kwa mapenzi na nidhamu ya hali ya juu napenda sana kuwa mwenye nidhamu katika tasnia yangu”, amesema Anthony Joshua.

Anthony Joshua ameingia ulingoni na kupigana mapambano 19 ambapo amefanikiwa kushinda yote 19 huku akiwapiga wapinzani wake kwa KO katika mapambano yote 19 bila kupoteza hata pambano moja.

Dondosha comments


Share this