KOCHA ATOA SIRI YA UKOMAVU WA CHRISTIANO RONALDO FERGUSON AHUSIKA

Share this

Mafanikio katika kazi yoyote ayawezi kuja bila changamoto mbalimbali ambazo kwa kawaida binadamu mwenye nia ya dhati ya kufikia malengo yake huwa atishwi na changamoto hizo kwasababu ndizo ambazo zinamjenga katika kile ambacho ana maono nacho kukifikia.

Kwenye mchezo wa soka kuna mambo mengi kwelikweli na baadhi ya wachezaji hushindwa kukabiliana nazo mfano mzuri ni kiungo fundi kutoka Tanzania naye si mwingine ni Haruna Moshi shabani (boban) yeye alipata nafasi katika timu kubwa mno kule nchini Sweden lakini kwa sababu ambazo zinazo julikana za kushindwa kuendelea kucheza Sweden ni baridi kali na kuwa mpweke pale ambapo anatoka mazoezini au kwenye mechi.

Mfano huo unatosha kabisa kuonyesha ni namnagani wachezaji kutoka Tanzania kushindwa kukabiliana na changamoto katika soka,wachezaji wengi kutoka Afrika Magharibi wanadiriki kuzamia nchi mbalimbali ili wapate  nafasi za kuonyesha vipaji vyao la hasha baadhi yao hukubali pia kucheza bila malipo huku wakiwa na malengo ya kufika pale ambapo wanapataka.

Katika soka lililo endelea kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson aliwaruhusu wachezaji wa Man United wakiwa mazoezini kumchezea vibaya mchezaji wa zamani wa timu hiyo Christiano Ronaldo ikiwa ni njia ya kumkomaza na kumundoa tabia yake ya kujiangusha,Siri hiyo amefichua  Tony Coton ambaye alikuwa kocha wa makipa katika klabu hiyo.

Amesema Ferguson aliwaelekeza wachezaji na benchi lake la ufundi kuwa Ronaldo achezewe faulo katika mazoezi na mechi za mazoezini kuondoa tabia ya kujiangusha chini ovyo,Coton anasema kuwa Fergie aligundua kuwa Ronaldo alipowasili Man United (2003) alikuwa mlegevu hivyo alitumia njia hiyo kumkomaza.Je wachezaji wetu wa Tanzania wataweza?

Dondosha comments


Share this