“MARA PAAAP”NIMEKUWEKEA HAPA TRAILER YA MOVIE MPYA YA EMINEM NI SHIDAA

Share this

Inawezekana soko la Movie likawa linalipa zaidi kuliko mziki baada ya kushuhudia wanamziki mbali mbali wakiingia kwenye tasnia ya movie,Baadhi ya wasanii ambao tumeona wameingia kwenye Movie ni 50 cent,Ice cube,Chris Brown na wengine kibao.

Sasa Good news ni kwamba msanii wa HipHop Eminem tayari amethibitisha kutoa Movie yake mpya ambayo kwa mara ya kwanza itaonyeshwa kwenye tamasha Toronto film festival mwaka 2017,Ndani ya filamu hiyo ambayo imepewa jina la Bodied ambayo ina maudhui ya mashindano ya rap komedi.

Movie hiyo ambayo imeongozwa na mkali Joseph khan imewajumuisha marapper wakali kama Loaded Lux, Dizaster, Dumbfoundead and Hollow Da Don wengine waliocheza ni Anthony Michael Hall, Debra Wilson, Charlamagne Tha God, Alter Perez, Rory Uphold, Jackie Long, Callum Worthy and Shoniqua Shanda,Eminem pia ametumia baadhi ya nyimbo zake kama sound track kwenye Movie hiyo huku akitumia baadhi ya midundo ya Dr Dre.

 

Dondosha comments


Share this